FISTON Mayele mshambuliaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anacheza ndani ya Pyramids ya Misri ameweka wazi kuwa mabosi wake wa zamani hao wana timu nzuri inayoonyesha ushindani kutokana na mwendo walionao katika mechi zao.
Ikumbukwe kwamba nyota huyo alikuwa chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi alikuwa anatajwa pia kuwa kwenye rada za Smba mpango huo ukabuma.
Septemba 29 2024 wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex ubao ukisoma Yanga 1-0 KMC kwa bao la ushindi likifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 4.
Ni pointi 9 wanafikisha Yanga baada ya kucheza mechi tatu na zote wameshinda huku safu ya ushambuliaji ikifunga jumla ya mabao manne kwenye mechi hizo kinara ni Maxi mwenye mabao mawili.
Mayele amesema; “Yanga wana kikosi kizuri na nimeona namna ambavyo wanacheza kwenye mechi za ushindani kila mchezaji anaonyesha kitu kizuri na hili ninafurahi kuona likiendelea kwa kuwa maisha ya mchezaji ni kucheza na ambacho kinahitajika uwanjani ni mataokeo.
“Nimeona mchezo dhidi ya KMC nilikuwa jukwaani hakika KMC walikuwa na siku nzuri kazini namna ambavyo walikuwa wakicheza kwa nidhamu na Yanga nao walicheza vizuri na mwisho wamepata ushindi hivyo ni ligi yenye ushindani kweli kwa kila timu.”