ALIYEWAHI kuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele anayekipiga katika klabu ya FC Pyramids ya Misri, amefunguka na kuelezea ugumu anaokutana nao huko Misri.
Mayele ameenda mbali zaidi na kusema kwamba anapenda kucheza Tanzania, kwani hapa ni kama nyumbani kwake.
Aliyasema hayo jana kweneye mchezo wa kimataifa kati ya Ethiopia na DR Congo, ambao ulimalizika kwa ushindi wa mabao 2, huku yeye akifunga bao moja.
“Siku zote kwangu ni furaha kucheza na ndugu zangu Tanzania ni nyumbani kwangu pia katika michezo yote miwili atakayejipanga vizuri ataibuka mshindi na kuhusu ligi ipi kati ya Tanzania na Misri.
Ligi ya Misri ni ngumu kuliko ya hapa Tanzania ninafuraha kuingia kwenye Historia ya Timu haijawahi kubeba kombe ila mimi nimeisaidia kuchukua kombe.