Bila shaka umewahi kuwaona wachezaji wengi wa Ulaya na hata wa hapa Tanzania kama Simba, Yanga, Azam na vilabu vingine vikubwa wakiwa wamevalia vest nyeusi vifuani mwao? umekuwa ukijiuliza hizo vest zinasaidia nini kwa mchezaji au umewahi kujiuliza vinafanya kazi gani kitaalam?
Majibu ni haya hapa;
Zile vest kitaalamu zinaitwa GPS VESTS. Lakini mara nyingi kifuani hua zinaandikwa Catapult au Fitogether ambao ndio watengenezaji wa hizi vest.
Catapult ni neno la kigiriki lenye maana ya manati!! Hizi vest zinaitwa hivyo kutokana na muundo wake kufanana na manati. (YES MANATI HAYA YA KUWINDIA)
Sasa tuangali je zinakazi gani?
Hizi vest hua ni maalumu kwa ajili ya kuwekea vifaa vya GPS tracker. Ambapo mchezaji akiivaa hii vest kwenye eneo la mgongo kuna ka eneo kadogo ambapo hio GPS tracker hua inapachikwa.
Je hizo GPS zinakazi gani?
GPS tracker kazi yake kubwa ni kufatilia mienendo ya mchezaji akiwa uwanjani. kwamaana kwamba Mchezaji akivaa hii GPS tracker, Benchi la ufundi linaweza kujua yafuatayo.
a) Amekimbia umbali gani uwanjani b) Amefika maeneo gani kwa sana uwanjani c) Amehusika mara ngapi kwenye matukio ya kimpira d) Nguvu alizotumia uwanjani Etc.
Ripoti hii inasaidia bench la ufundi kujua mwenendo wa kikosi chao na sehemu za kuboresha hasa kwenye eneo la kiufundi pamoja na physique ya mchezaji.
Sasa mtu anaweza kuuliza kama hizo GPS hazimuumizi mchezaji awapo uwanja kama akidondoka au anavokimbia.
Jibu ni Hapana haviumizi kwasababu hizo vest zimetengenezwa kwa material maalumu ambayo yanamlinda Mchezaji kutodhurika na hivi vi GPS na ndio maana eneo la kukaa hio GSP in juu ya mgongo sehemu ambayo ni ngumu kufikika hata ikitokea mchezaji anaudondoka.