KUHUSU SIMBA,YANGA KUFUZU KIMATAIFA…FAIDA MPYA KWA TANZANIA HIZI HAPA
Na: Hashim Mbaga
TUNAENDELEA KUTOA UFAFANUZI
Katika Misimu Yote 8 ambayo inatumika Ranking Point toka 2018 hadi 2024-2025, Tanzania tumeweza kushiriki Misimu 7 Katika nafasi 11 Tofauti Tofauti kwa Timu Tatu ambazo ni Namungo, Yanga na Simba.
Timu Ya Namungo katika Msimu wa 2020-2021 iliweza kuingia Group Stage ya Confederation Cup na kuweza kupata Point 2.5 ambazo kila msimu unafuata ziliendelea kupungua mpaka msimu huu wa 2024-2025 zimebaki Point 0.5 tu.
Timu ya Yanga katika msimu wa 2018 iliingia Group Stage Confederation Cup na kupata Point 2.5, Msimu wa 2022-2023 ikaweza kuingia Fainali Confederation Cup na kuweza kupata Point 20, Msimu wa 2023-2024 ikaweza kuingia Quarter Final Champions league na kuweza kupata Point 15 na Msimu huu wa 2024-2025 ndio imeanza na kuingia Group Stage Champions league na kupata Point 5.
Jumla Yanga kwa muda wote katika kushiriki mara 4 iliweza kutengeneza jumla ya Point 42.5 zilizotoka na za Mwanzo 2.5, zile za Pili 20, zile za Tatu 15 na sasa Mpya 5 ambazo kila msimu zitapungua, mfano Point za Msimu ulioisha 2023-2024 ambazo ndio zitatumika katika upangaji msimu huu zipo Point 31 zilizotokana na Zile za mwanzo kufutika zote, zile za Pili kubaki 16 na za Tatu kuwa 15 ndio zinafanya Point 31 ila baada ya kuanzia msimu huu wa 2024-2025 zinapungua na kubaki Point 29 anazoendelea nazo sasa ambazo zimetokana na zile za pili 20 zimebaki 12, zile za Tatu 15 zimebaki 12 zilizozalisha jumla Point 24 na sasa Mpya 5 kufanya Jumla ya Point 29.
Timu ya Simba katika msimu wa 2018-2019 iliingia Group Stage Champions league na kupata Point 15, msimu wa 2020-2021 ilingia tena Group Stage Champions league na kupata Point 15, Msimu wa 2021-2022 ikaweza kuingia Quarter Final Confederation Cup na kuweza kupata Point 10, Msimu wa 2022-2023 ikaweza kuingia Quarter Final Champions league na kuweza kupata Point 15, Msimu wa 2023-2024 ikaweza kuingia Quarter Final Champions league na kuweza kupata Point 15 na Msimu huu wa 2024-2025 ndio imeanza na kuingia Group Stage Confederation Cup na kupata Point 2.5
Jumla Simba kwa muda wote katika kushiriki mara 6 iliweza kutengeneza jumla ya Point 72.5 ambazo kila msimu zitapungua zilizotokana za Mwanzo 2.5, zile za Pili 15, zile za Tatu 15, zile za Nne 10, zile za Tano 15 na sasa Mpya 5 ambazo kila msimu zilipungua, mfano Point za Msimu ulioisha 2023-2024 ambazo ndio zitatumika katika upangaji msimu huu zipo Point 39 zilizotokana na Zile za mwanzo kufutika, zile za Pili kubaki 6 na za Tatu kubaki 6, zile za Nne kubaki 12, zile za Tano kubaki 15 ndio zinafanya Point 39 ila baada ya kuanzia msimu huu wa 2024-2025 zinapungua na Sasa kubaki Point 30.5 anazoendelea nazo ambazo zimetokana na zile 15 za mwanzo zimefutika zote, zile 15 za pili zimebaki 3, zile 10 za tatu zimebaki 4, zile 15 za Nne zimebaki 9, zile 15 za Tano zimebaki 12 zilizozalisha jumla Point 28 na sasa Mpya 2.5 kufanya Jumla ya Point 30.5
Mfumo huu upo ndani ya Miaka mitano ya Ufanisi wa Timu na Point zinahesabiwa kwa kiwango ulichopata baada ya kutoka/kuishia kuzidishwa kwa mwaka ambao umecheza kuanzia mwaka wa mwisho alama 1 hadi mwaka unacheza sasa alama 5, Kila mwaka au msimu unavyosogea mbele ina maana hesabu inabadilika maana ile miaka Mitano nayo inasogea na kuacha ule wa mwisho kufutwa.
Hii ndio inapelekea Kila msimu Point kubadilika maana alama za Miaka katika kuzidisha zinabadilika sababu ya kusogea mbele mwaka mmoja kila msimu mfano kama sasa una Point 1 urazidishiwa mara 5 ila mwakani kwa Point yako 1 itazidishwa mara 4 hivyohivyo 3 na 2 mpaka mara 1 mwisho inafutwa.
Draw inayoenda kufanya 07/10/2024 kupanga Group Stage kwa Champions league na Confederation Cup zinatumika Point zilizozalishwa miaka Mitano ya toka 2019-2020 hadi msimu ulioisha 2023-2024, ambako Yanga wana Point 31 wakiwa nafasi ya 13 na Simba wana Point 39 wakiwa nafasi ya 7.
Hizi Point zinazozalishwa sasahivi ni kwa ajili ya kuhesabiwa msimu ujayo 2024-2025 sio sasahivi, ndio maana unaweza kuona hazijawa Fixed hazijatulia zinakuwa kama Live score ambako sasa ndio zinaonyesha Yanga ana Point 29 nafasi ya 11 na Simba Point 30.5 nafasi ya 8 zitaendelea kubadilika kadiri timu hizi zitavyoendelea kushiriki na kupata matokeo yao mpaka mwisho ndio Ranking halisi itakaa na kuweza kuhesabiwa.
PLAY FAIR, BE POSITIVE