Hakuna Ubishi kwamba Yusuph Kagoma alikua na mkataba na timu yake ya Singida Fountain Gate. Hivyo ilibidi ufanyike uhamisho kwa kumnunua kwenda timu nyingine yeyote.
Mkataba wa kumnunua unaonesha ni wa pande tatu, Yanga, Singida na Kagoma mwenyewe. Hata hivyo mkataba huo una mapungufu yafuatayo.
1. Japo unaonekana kuwa wa pande 3, hauoneshi Kagoma kusaini mkataba huo.
2. Mkataba huo unasema Yanga ndiye anayemuuza Kagoma Kwenda Singida.
Malipo ya Ada ya Uhamisho: Kipengele namba 3.1 cha Mkataba wa uhamisho unaonesha malipo yatalipwa kwa awamu 2 zilizo sawa, Aprili na June. Risiti ya malipo inaonesha tu 30M zote zimelipwa April 30 bila kueleza wanalipia nini.
Ikumbukwe pia muda huohuo inadaiwa waliingia makubaliano ya kumnunua kibabage kwa 30M.
Yanga walimsainisha Kagoma, kipengele namba 2 cha mkataba huo kinasema mkataba utakua valid endapo registration ya mchezaji itakamilika kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Kwahiyo, mkataba huo ulikua unakamilishwa na usajili wa mchezaji kwenye Mfumo ( ukizingatia Yanga alikua amefungiwa kusajili pia, angalia viambatinishi taarifa za TFF za kufungiwa na kufunguliwa kusajili)
Kuna barua ya Singida ya Tar 6 Mwezi wa 7 ikiwataarifu Yanga kuvunja mkataba kwa kushindwa kulipa, Barua hiyo inaonesha Singida kukubali kupokea malipo ya 30M ambayo ni kwa ajili ya kumnunua Kibabage, ambaye kwa muda huo alikua tayari ameshataambulishwa Yanga (4 July, 2024).
Yanga Baada ya Barua hiyo ndio wakakimbia kulipia 30M nyingine tarehe 7 Julai na kuwaomba Singida wawape release ya Kagoma. Wakati wanafanya hayo mchezaji na Singida walikua washamalizana na Simba na release letter ilishatoka kwa mchezaji kujiunga na Simba.
Mchezaji hakujipeleka Simba, aliuzwa . Simba ikafanya taratibu za Usajili na Kupata Leseni.
Mkataba wa Kagoma na Yanga (ambao ungekua halali endapo Registration ingekamilika) unaeleza wazi kuwa Mgogoro wowote utapelekwa FIFA Dispute Resolution Chamber.
Kwa Yanga kupeleka Mgogoro huo TFF ni kukiuka Mkataba ambao wao wenyewe wanadai Kagoma amevunja.
Narudia kusema hapa kuna kesi ya MADAI hakuna kesi inayohusiana na usajili, Fontain Gate watoke waseme na wao.
Ameandika Jemedari Kanzumari.