Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Feisal Salum Abdallah (Fei Toto) amepiga chini ofa ya pili kutoka Azam ambayo ilimtaka kuongeza mkataba mpya. Kwa sasa Fei Toto anahitaji changamoto mpya ndani au nje ya nchi
Azam wanajiandaa kuweka ofa Nyingine mezani ili kumbakisha Fei Toto,na ofa hiyo mpya inatarajiwa kuwekwa Mezani wiki hii ambapo viongozi watatu wa juu wa Azam watakaa kikao na Fei Toto pamoja na wakala wake Hafidh.
Kusema ukweli Asilimia za Fei Toto kubaki Azam ni chache sana unless Azam wakubali kumlipa Fei Pesa chafu…..Ikumbukwe kwa sasa Fei analipwa Tsh 23m kwa mwezi.
Zaidi ya Mara mbili viongozi wa Simba walifanya mazungumzo na Fei Ila dili Hilo halikufanikiwa kukamilika,huku Mara ya Mwisho Try Again akikutana uso kwa uso na Nyota huyo pale Zanzibar wakati Azam wanajiandaa na msimu mpya.
Hivi sasa viongozi wa Yanga wanafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Fei huku wakiamini Nyota huyo anaweza kurejeshwa jangwani mwishoni mwa msimu huu.
Ni wazi Fei Toto anakwenda kuziweka vitani Simba na Yanga.
Source: Hans Raphael.