Usiku wa kuamkia leo mataifa mawili makubwa kwenye soka kutokea Bara la Amerika Kusini Brazil na Argentina yamechezea vichapo kwenye michezo ya kufuzu Kombe la Dunia inayoendelea Barani humo.
Mapema kabisa ilikuwa Argentina ambao wao wamejikuta wakichapwa goli 2-1 na timu ya taifa Colombia kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Estadio Metropolitano Roberto Meléndez huko Barranquilla nchini Colombia.
Magoli ya Colombia yamefungwa na Yerson Mosquera pamoja na James Rodriguez huku lile la Argentina likifungwa na Nicolás González.
Majira ya saa 9:30 usiku kwenye dimba la Estadio Defensores del Chaco huko Asunción, Paraguay wakiwa wenyeji wakaikaribisha Brazil.
Bao la Diego Gomez anaecheza Inter Miami ya Marekani kwenye dakika ya 20 likawaangamiza Brazil na kushuka hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wakiwa na alama zao 10 sawa na Venezuela ambao wako nafasi 6.
Argentina licha ya kupoteza wameendelea kusalia kileleni wakiwa na alama zao 18, Colombia yuko nafasi ya pili akiwa na alama 16, Uruguay wako nafasi ya tatu wana alama 15 Ecuador yuko nafasi ya nne wana alama 11.