LEGEND kwenye ulimwengu wa Habari za Michezo Bongo, Saleh Ally Jembe ameweka wazi kuwa beki chipukizi kutoka Rwanda ambaye anacheza ndani ya kikosi cha Al Ahli Tripoli ni mchezaji wa Hovyo kutokana na vitendo vyake kutokuwa vya kiungwana.
Ikumbukwe kwamba Al Ahli Tripoli imefungashiwa virago na Simba ya Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho hatua ya raundi ya pili kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1.
Jembe amesema kuhusu beki huyo Thierry Manzi namna hii: ” Manzi ni beki anayechipukia kutoka nchi jirani ya Rwanda ambayo inapambana kukuza wachezaji anakipiga Al Ahli Tripoli iliyotolewa na Simba.
“Nimemshuhudia katika mechi mbili dhidi ya Simba, hakika ni mpambanaji lakini ni mchezaji mwenye tabia ya HOVYO SANA.
“Anataka KUWAVUNJA wachezaji wengine kwa MAKUSUDI. Katika mechi mbili dhidi ya Simba amefanya hivyo mara nne. Si alikuwa anaokoa, au bahati mbaya na wazi inaonyesha ANATAKA KUUMIZA, jambo ambalo linapoteza ile kariba ya professionalism kwa kuwa kama unaona sahihi kumuumiza mwenzako kwa hila au makusudi basi hutambui maana ya soka upendo, soka ajira au soka ni ndoto za maisha ya wanasoka maana hiyo ni kazi na ndio wanaitumia kuendeshea maisha na nini maana ya UMUHIMU WA KULINDANA…
“Rwanda wanamtegemea ila ili aende mbali zaidi LAZIMA ABADILIKE.”
Mchezo wa kwanza ugenini ilikuwa 0-0 na mchezo wa pili uliochezwa Uwaja wa Mkapa Septemba 22 baada ya dakika 90 ilikuwa Simba 3-1 Al Ahli Tripoli.