Klabu ya Barcelona imekamilisha usajili wa aliyekuwa kipa wa klabu ya Arsenal, Juventus na timu ya taifa ya Poland Wojciech Szczesny kwa mkataba wa mwaka mmoja kuziba nafasi ya kipa wao namba moja Mjerumani Marc Ter Stegen aliyeumia.
Szczesny aliyekuwa kwenye mipango ya kustaafu soka amelazimika kukubali ofa ya Barcelona ambayo itamkosa Ter Stegen kwa zaidi ya miezi 8.
Szczesny anajiunga Barca akiwa mchezaji huru.