Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekubali kusaini kandarasi mpya ya miaka 3 itakayomuweka kwenye Uwanja wa Emirates hadi mwaka 2027 ambapo Mkataba wa awali wa Arteta ulikuwa unatamatika mwishoni mwa msimu huu.
Katika Msimu uliopita Arsenal Arterta alianza kwa ushindi wa pili wa Ngao ya Jamii ya FA na kumaliza msimu wakiwa wapili kwenye Ligi Kuu ya England, huku timu hiyo ikihakikisha inakuwa kwenye mbio za ubingwa hadi siku ya mwisho.
Katika msimu uliopita, Aliweka rekodi nyingi za klabu ikiwa ni pamoja na kushinda mechi nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu England (28), mabao mengi zaidi ya Ligi Kuu (91) na kiwango cha juu zaidi cha ushindi kwa jumla (67.3%) hiki kikiwa kikubwa katika historia ya Arsenal. Mikel aliteuliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi kwenye Ligi Kuu ya England kwa mara saba.
Pia aliiwezesha Arsenal kufuzu Ligi ya Mabingwa UEFA baada ya kukosekana kwa miaka saba
Mwenyekiti Mwenza wa Arsenal, Josh Kroenke, alisema: “Tunafuraha kwa kuongeza mkataba wa Mikel.
“Mikel ni meneja mahiri na mwenye shauku, ambaye ni mtu asiyechoka katika kutafuta ubora. Ana ufahamu wa kina wa maadili ya Arsenal, na tangu ajiunge nasi kama Kocha Mkuu mnamo Desemba 2019, ameipeleka timu kwenye kiwango kingine kwa njia ya Arsenal.
“Kuna hali nzuri ya pamoja ya timu katika klabu, na kwa uhusiano mkubwa tulionao kati yetu na imani katika kile tunachofanya, tunatazamia kwa furaha na kujiamini, tunapoendeleza lengo letu – kushinda pamoja.”