MENEJA wa Yanga SC, Walter Harson ameweka wazi kuwa maandalizi yanaendelea vizuri nchini Afrika Kusini kwa ajili ya msimu wa 2024/25 kwa kuwa wachezaji wapo vema.
Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ipo kambini Afrika Kusini kwa maandalizi ya mechi za kitaifa na kimatafa ambapo Yanga inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Leo Julai 24 2024 Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa pili wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya TS Galaxy unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Meneja amesema: “Wachezaji wapo vizuri kwa ajili ya mchezo wetu wa kirafiki isipokuwa Boka Chadrack ndiye mchezaji ambaye bado hayupo sawa kujiunga na wenzake kwenye mchezo wa Mpumalanga Premier’s International Cup 2024 dhidi ya TS Galaxy.
Gamondi amesema kuwa mechi ambazo wanacheza kwa sasa ni maandalizi ya kikosi hicho kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Mchezo wa kwanza ilikuwa Julai 20 2024 ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-2 FC Augsburg hapo ndipo Boka alipata maumivu kwenye mchezo huo.