“Wengi wanauliza mpaka sasa tumenufaika vipi na utambulisho wa Chama. Mpaka sasa tumepokea taarifa za mashabiki wa upande wa pili ambao wamehamia Yanga akiwemo Baba Kamwe nae amemfuata Chama. Wote waliohama tunawaandalia siku maalumu ya kuwapokea”
“Suala la Usajili wa Chama ni sehemu ya biashara yetu. Kila mtu anakiri kuwa usajili wa Chama ni usajili mkubwa. Najua wengi wanauliza kwanini hatujamtambulisha Chama na jezi ya Yanga. Mtiririko wa matukio ya usajili huu wa Chama kwetu ni fursa. Najua wengi wanatamani kujua Chama ataonekanaje na jezi ya Yanga. Hapo ndipo tunalenga kuuza usajili huu”.
Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe