KIMATAIFA

UHISPANIA YATWAA UBINGWA WA EURO KWA MARA YA NNE

Uhispania imetwaa ubingwa wa kombe la Mataifa Ulaya, EURO kwa mara ya nne kihistoria kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya England kwenye fainali katika dimba la Olympiastadion (Berlin).

Hispania walitwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza mnamo 1964 kabla ya kutwaa mara mbili mfululizo mwaka 2008 na 2012 na leo wametwaa kwa mara ya nne.

FT: Uhispania 🇪🇸 2-1 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 England

⚽ Williams 46’

⚽ Oyarzabal 87’

⚽ Palmer 72’

England inaendelea kusubiri ubingwa wake wa kwanza wa EURO baada ya kupoteza fainali yake ya pili mfululizo baada ya kupoteza EURO 2020 dhidi ya Italia, leo tena wameangukia pua.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button