KITAIFA

UCHAMBUZI WA AHMED ALLY KUHUSU ‘MUTALE’

Baada ya usajili wa Joshua Mutale Semaji la CAF, Ahmed Ally ametamba kuwa mabeki wa timu pinzani kwenye ligi na kimataifa wajipange kwa ubora wa nyota huyo walimempa mkataba wa miaka mitatu.

Kiungo mshambuliaji huyo atavaa ‘ngozi’ ya Simba kwa msimu wa 2024/25 wa Ligi Kuu na kimataifa baada ya kusaini mkataba huo akitokea klabu ya Power Dynamos ya Zambia.

Uwezo wa kiungo huyo wa kucheza nafasi zote na kasi yake kama treni ya SGR unahitaji mabeki wa timu pinzani akiwemo mabeki wa Yanga, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Yao Attohoula kujipanga vizuri kumdhibiti.

Akizungumza nasi, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema Joshua anaweza kumudu nafasi ya winga ya kulia na kushoto wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji.

Amesema mabeki wa timu pinzani wanatakiwa wajipange vizuri kwa sababu ya kasi na ubora wa nyota huyo anayemudu kucheza nafasi nyingi uwanjani, itawatesa sana.

“Simba tumemsajili Joshua akiwa Power Dynamos msimu uliopita, amefunga mabao nane na kusaidia kupatikana kwa mengine 10 katika michezo 26, uwezo wake wa kumudu kucheza nafasi nyingi uwanjani pamoja na umri mdogo ni miongoni mwa vigezo vilivyotuvutia kumsajili huyo mchezaji ikiwa ni mikakati maalum ya kuboresha kikosi kwa kusajili damu changa,” amesema Ahmed.

Amesema wachezaji walio nje ya nchi wameshaanza kuwasili nchini na waliopo mikoani watafika mapema na kuingia kambi ya mwanzo kabla ya kwenda Misri, kila kitu kinaenda vizuri na wiki hii wako “busy” na kutambulisha wachezaji pamoja na benchi lote la ufundi ikiwemo kocha mkuu na wasaidizi wake.

“Tunatarajia kuondoka nchini kuanzia Juali 7, mwaka huu kwenda Misri, kwa ajili ya Pre Season na tayari wachezaji wameanza kuwasili Tanzania kwa wakigeni na waliopo mikoani nao wameanza kuja Dar es Salaam. kuanza kupima afya ikiwa kawaida ya wachezaji wanapoanza msimu kupima kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano,” alisema Ahmed.

Inadaiwa Simba imekamilisha usajili jumla ya wachezaji nane akiwemo Jean Ahoua, Elie Mpanzu, Debora Fernandez, Valentin Nouma, Agustine Okejepha

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button