Paris St-Germain wakubali dili na Jadon Sancho, Manchester United wanaweza kumlenga Nordi Mukiele, Manuel Ugarte au Milan Skriniar katika mpango wa uhamisho utakaohusisha kubadilishana na Sancho, West Ham wanaanza mazungumzo juu ya uhamisho wa Aaron Wan-Bissaka.
Paris St-Germain wana makubaliano ya awali na mshambuliaji wa Uingereza Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 24, lakini lazima wafikie bei inayotakiwa na Manchester United ya takriban £50m. (Sports Zone – kwa Kifaransa)
United inaweza kumlenga beki wa kulia wa Ufaransa Nordi Mukiele, 26, 23, kiungo wa kati wa Uruguay Manuel Ugarte au mlinzi wa kati wa Slovakia Milan Skriniar, 29, katika mpango wa kubadilishana na Sancho. (Express)
West Ham wameanzisha mazungumzo juu ya mkataba wa beki wa kulia wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka kutoka Manchester United , ambaye thamani yake ni ya zaidi ya £15m. (Sky Sports)
Chelsea imefanya mawasiliano na mshambuliaji wa Juventus na Italia Federico Chiesa , 26 , ambaye pia anasakwa na Tottenham (Team talk)
Genoa bado wanashinikiza kupata mkataba na mlinda lango wa zamani wa Uhispania David de Gea, 33, ambaye hajacheza tangu aondoke Manchester United Julai 2023. (Football Italia)
Matarajio ya mshahara wa De Gea, hata hivyo, yanaonekana kuwa kikwazo katika mazungumzo. (Sky Sports)
Aston Villa wamewasilisha ofa ya mkopo kwa kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips, 28(Football Insider).
Everton wamekubali mkataba wa takriban pauni milioni 22 kumsaini beki wa Jamhuri ya Ireland Jake O’Brien, 23, kutoka klabu ya Ufaransa ya Lyon . (Sky Sports)
Winga wa Crystal Palace Muingereza Jesurun Rak-Sakyi, 21, anapendelea kuhamia Southampton kuliko Leeds msimu huu wa joto. (Football Insider)
West Ham wako tayari kukidhi hitaji la bei ya AS Monaco la euro 35m (£29.5m) kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Youssouf Fofana, 25. (L’Equipe – kwa Kifaransa)
Fofana ana makubaliano ya mdomo ya kujiunga na AC Milan . (Sky Germany)
AC Milan wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili beki wa Brazil Emerson Royal, 25, kutoka Tottenham . (Fabrizio Romano)
Arsenal are in pole position to sign Sweden forward Viktor Gyokeres from Sporting Lisbon, with Liverpool not prepared to submit a bid for the 26-year-old. (Team talk)
Arsenal wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres kutoka Sporting Lisbon, huku Liverpool wakiwa hawajajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Team talk)