Kiungo kinda wa Azam FC, Adolf Mtasingwa ameomba kuvunja mkataba katika klabu yake hiyo yenye maskani yake Chamazi, Dar es Salaam.
Inelezwa kuwa, Adolf ameueleza uongozi wa Azam FC kuwa amepata timu nje ya nchi. Adolf amebakiza mkataba wa miezi sita (6) katika klabu hiyo.
Azam FC wanataka walipwe Tsh 790 million (USD $ 300,000) pesa ambayo ipo Kwenye mkataba wake (Release clause).
Inaelezwa kuwa Klabu ya Yanga iko nyuma ya dili hilo kwani imekuwa na malengo ya kumnyakua kijana huyo aliyepandishwa kutoka timu ya vijana ya Azam.