Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephan Aziz Ki amethibitisha kuwa ataendelea kukipiga mitaa ya Twiga na Jangwani msimu ujao licha ya kuwa na ofa nono kutokea CR Belouizdad ya Algeria.
Nyota huyo ambae alijiunga na Yanga SC mwaka 2022 alikuwa akiwaniwa pia na Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates, Kaizer Chiefs na baadhi ya klabu nyingine kutokea kaskazini mwa Afrika.