KITAIFA

SIMBA YATAMBA KUSHUSHA MASHINE MPYA ZA KAZI

UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa wachezaji wapya ambao wametambulishwa watafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wengine katika mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

Simba imeweka kambi nchini Misri ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kujipanga kufanya vizuri.

Ipo wazi kwamba katika anga la kimataifa Simba itashiriki Kombe la Shirikisho baada ya kugotea nafasi ya tatu kwenye msimamo na namna nne ni Coastal Union ambayo iligotea nafasi ya nne.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani utakuwa mkubwa hilo linawapa nguvu wachezaji kuongeza juhudi kwenye maandalizi.

“Wachezaji wetu wote wapya na wale waliokuwa kwenye kikosi msimu wa 2023/24 wapo imara na wanatambua kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya. Tunaelekea kwenye Simba Day Agosti 3 2024 hii ni siku muhimu kwetu na Wanasimba mjitokeze kwa wingi kwa kuwa kuna mashine za kazikazi.”

Wachezaji waliopo kambini ni pamoja na Mukwala Steve, Awesu Awesu. Willy Onana, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button