UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa uzinduzi wa Simba Day 2024 utafanyika Morogoro na safari inatarajiwa kuwa Julai 24 2024 kwa mashabiki na viongozi kuelekea mji kasoro bahari.
Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa lengo kubwa ni kuendeleza utofauti ambapo watafanyia uzindi kwenye hifadhi ya Mikumi kuhamashisha utalii kwa Watanzania wote kwani sio gharama kubwa kufika hapo kwa Watanzania.
“Twendeni Hifadhi ya Mikumi tukawaonyeshe Watanzania kuna hifadhi, ni karibu na kiingilio ni 5,900. Kuna wengine wakisikia utalii wanajua ni mamilioni kumbe ni hela kidogo. Lakini pia ni kwenda kutangaza treni mpya ya SGR. Kwanza ni bidhaa mpya ambayo inatakiwa kutangazwa na sisi Simba ndio Wenye Nchi kuitangaza.
“Julai 27 itakuwa Simba Week Bonanza pale uwanja wa Mwembe Yanga Temeke. Julai 28 tutakuwa Mbagala, huwezi kufanya Simba Week bila kufika Mbagala, tutakwenda kuliamsha. Ndani ya wiki hii tutafanya kwanza burudani, kurudisha kwa jamii. Kila Mwanasimba, kila tawi wahakikishe wanajikusanya kwenda kutoa misaada.” Amesema Ally.
VIINGILIO VYA SIMBA DAY 2024
Mzunguko – Tsh. 5,000
Machungwa – Tsh. 10,000
VIP C – Tsh. 20,000
VIP B – Tsh. 30,000
VIP A – Tsh. 40,000
Platinum – Tsh. 200,000.