Timu ya Taifa ya Colombia imetinga fainali ya michuano ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay goli 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa kwenye uwanja wa Bank Ofa America huko Charlotte NC.
Bao la Colombia limewekwa kambani na nyota wa Crystal Palace ya Uingereza Jefferson Lema dakika ya 39 akimalizia pasi safi ya James Rodriguez.