MABINGWA WA BONGO WAIVUTIA KASI KAIZER CHIEFS
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/24 Yanga wapo tayari kuwakabili Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa Toyota Cup.
Yanga wapo katika viwanja vya St Stithians, Johannesburg, Afrika Kusini chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuinoa timu hiyo kwenye mechi za ushidani.
Julai 28 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuanza Agosti 16.
Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi ni Clatous Chama, Pacome, Aziz Ki, Prince Dube, Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Yao, Jean Baleke.
Kwenye mechi mbili zilizopita za kirafiki, Yanga ni nyota wawili walipata nafasi ya kufunga ambao ni Jean Baleke kwenye mchezo wa kwanza na mchezo wa pili ni Prince Dube alipata nafasi ya kufunga.
Gamondi amebainisha kuwa mechi za kirafiki ambacho kinatazamwa kwa ukaribu ni namna wachezaji wanavyotumia maelekezo wanayopewa ili kuwa imara na kufanyia kazi makosa yao zaidi kuliko kufikiria ushindi.
“Kwenye mechi zetu za kirafiki kikubwa ambacho tunakitazama ni namna wachezaji wanavyocheza na kutumia maelekezo ambayo tunayafanya katika eneo la mazoezi hivyo kushinda kwetu sio kipaumbele kikubwa.’