CECAFA IMEFIKA PATAMU, RAIS AZUNGUMZIA TIMU AMBAZO HAZIJASHIRIKI
RAIS wa CECAFA, Wallace Karia amebainisha kuwa mashindano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup 2024 yamekuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikifanya kweli katika mashindano hayo. Kwa Tanzania Simba, Yanga na Azam FC zilipewa mualiko wa kushiriki mashindano hayo lakini hazikuwa sehemu ya washiriki.
Ikumbukwe kwamba kwa sasa timu nyingi zipo kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 kwa Bongo unatarajiwa kuwa ni Agosti 16 kwa timu kurejea uwanjani kwa ajili ya kupambania kombe.
Kesho Julai 19 2024 nusu fainali mbili zinatarajiwa kuchezwa viwanja viwili tofauti ni APR v Al Hilal itachezwa Uwanja wa KMC, Ali Wadi v Red Arrows huu utachezwa Uwanja wa Azam Complex.
Karia amesema: “Mashindano ya CECAFA haya yamefika hatua ya nusu fainali na kesho kutakuwa na mechi mbili zitakazochezwa viwanja viwili tofauti hii ni kubwa na mashindano yamefika kwa wakati muafaka.
“Mashindano ya vijana yatafanyika Uganda na vijana chini ya miaka 20 yatafanyika Tanzania, Tanga mashindano ya U 23 yatafanyika Ethiopia.
“Tunawaomba turudi tuwe timu moja na watu wanapaswa kujua kwamba mashindano ya CECAFA yanafanyika na kwenye Zone ambayo yanafanyika mashindano ya vijana sisi tumekuwa tukifanya vizuri zaidi.
“Haya mashindano tumeyafanya ni sehemu ya kuziandaa timu zetu hasa ukizingatia kwamba mashindano yamefanyika kwa muda mfupi ikiwa ni baada ya ligi kuisha tunaamini kwamba watatumia mashindano haya kwenda kurekebisha makosa ambayo yalitokea.
“Zone yetu ina nafasi ya timu nne na timu zote ambazo zipo lakini mimi na wenzangu tunaona kwamba CECAFA tumefanikiwa kuziandaa timu zetu. Haya mashindano hayajafanyika kwa muda mrefu hivyo kwa namna ambavyo yamefanyika imekuwa ni fursa kwa wengi kuona burudani.
“Tumejitahidi sana kuona haya yanafanyika hivyo kama kuna mtu alikuwa amepanga ratiba zake na hakuweza kushiriki hatuwezi kumlaumu kwa kuwa mashindano ya mwaka huu yamekuwa na ladha kubwa na ushindani mkubwa. Hata magoli yaliyofungwa ni historia niseme tu kwa wale wanaopenda timu zaidi kuliko mpira hao wanaweza kusema hayana ladha.”
One Comment