Yanga SC na Singida Black Stars zinatajwa kuwa kwenye vita nzito ya kuwania saini ya mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Jean Othus Baleke.
Inaelezwa kuwa Yanga SC wanahitaji saini ya Baleke baada ya Dili ya Jonathan Sowah kuwa ngumu Kwa upande wao.
Singida Black Stars wao wapo kwenye mikakati wa kuhakikisha wanatengeneza timu yenye ushindani kuelekea msimu ujao na Baleke anaonekana mtu sahihi wa kwenda kusimama kwenye ushambuliaji wa timu hiyo.