Timu ya taifa ya Argentina imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Copa America baada ya kuichapa Canada 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo.
Magoli ya Argentina kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja MetLife huko Eastern Rutherford nchini Marekani yamefungwa na Lionel Messi na Julian Alvarez.
Sasa Argentina anasubiri mshindi kati ya Uruguay dhidi ya Colombia unatarajiwa kupigwa usiku wa kuamkia kesho.