Kumekuwa na sintofahamu juu ya kusalia kwa Tanzania one Aishi Manula katika kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba, huku tetesi zikimuhusisha kuwa huwenda akarejea tena katika kikosi cha matajiri wa Dar es salaam Azam Fc.
Hivi karibuni mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi Simba SC na mshauri wa rais wa Simba Cresentius Magori akizungumza na Azam Tv amefunguka kuwa mpaka sasa Manula ni mali ya Simba.
“Manula bado ni mchezaji wa Simba na siwezi kulizungumzia hili sana, kwa sababu halipo chini yangu labda mtendaji mkuu wa klabu ndio anaweza kulieleza kwa usahihi na jana alikutana na mchezaji huyo”.
.
“Ila ninachofahamu ni mchezaji wa Simba kama kutakuwa na mabadiliko ufafanuzi utatolewa”.
Cresentius Magori Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, aliyewahi kuwa CEO wa klabu hiyo.