KITAIFA

YANGA, SIMBA, AZAM ZAPEWA TP MAZEMBE, RED ARROW NA WABABE WA SUDAN

TIMU za Tanzania zinazoshiriki michuano ya Caf zitapata nafasi nzuri ya kujiandaa na msimu mpya kwa kucheza na timu za Zambia, Sudan, Rwanda, Kenya na Uganda.

Habari za uhakika zinaonyesha Yanga, Azam, Simba na Coastal Union zitashiriki michuano ya Cecafa dhidi ya timu kutoka katika mataifa hayo. Cecafa ni Baraza lenye wanachama 12 ikiwemo Zanzibar.

Timu hizo nne zitakazoshiriki Caf Champions na Caf Confederation Cup zitacheza dhidi ya Al Hilal, Al Merreikh na Hai Ak Wadi za Sudan, Red Arrow ya Zambia na TP Mazembe ya DRC.

Michuano hiyo ambayo itakuwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya zitashirikisha timu 16 na itapigwa Tanzania.
Timu nyingine ni Nyasa Big Bullets ya Malawi, SC Villa ya Uganda, APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Vital’O (Burundi), JKU (Zanzibar) na El Merreikh Bentiu (Sudan Kusini).

Hivyo itakuwa ni sehemu ya maandalizi kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa kwa kutambua wapi wanapaswa kufanyia maboresho zaidi ili kuleta upinzani kwenye anga la kimataifa.

Ipo wazi kwamba Coastal Union ya Tanga na Simba ya Dar hizi zipo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku Yanga na Azan FC zote za Dar zipo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Matajiri wa Dar, Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Yusuph Dabo ni nafasi ya pili kwenye msimamo walimaliza ndani ya ligi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button