KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz amesema kama straika Prince Dube atatua kwenye timu yao, basi mashabiki wasahau suala ya kuwa mfungaji bora msimu ujao, badala yake amempa nafasi kubwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa ana mgogoro wa kumkataba na klabu yake ya Azam FC.
Maneno ya kiungo huyo raia wa Burkina Faso, yanaashiria kuwa huenda Mzimbabwe huyo akavaa jezi za njano na kijani msimu ujao.
Hata hivyo, Dube aliyeingia sintofahamu na viongozi wa Azam FC, kwa kuvunja mkataba wake kati kati ya msimu uliomaliza, anahusishwa na klabu mbili kubwa nchini Simba na Yanga.
Aziz Ki amefichua kuwa Dube huenda akawa ni sehemu ya usajili mpya ndani ya Yanga, akiamini kama atatua, atachukuwa nafasi katika eneo la ushambuliaji.
Amesema kama iwapo atajiunga na Yanga, anamtaka awe mfungaji bora kwa msimu ujao wakati yeye na viungo wengine kazi yao kubwa kuwalisha washambuliaji na mshambuliaji huyo atashirikiana na Joseph Guede.
“Sina uhakika wa kuchukuwa mfungaji bora msimu ujao, uhakika uliopo wa kuwa kinara wa ‘Assist’, wasahau kuhusu Aziz Ki kutwaa tuzo ya ufungaji bora mwa msimu ujao kwa sababu tayari ameletwa Dube,” amesema kiungo huyo.
Maneno hayo yaAziz Ki, yanathibitisha kuwa naye atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa msimu ujao na kuahidi kufanya kweli licha ya kuwa amekuwa anahusishwa kuondoka kwenye kikosi hicho, Malelodi Sundowns na Orlando Pirates za Afrika Kusini na Al Ahly ya Misri, zikitajwa kumhitaji.
Kiungo huyo amemnaliza msimu wa 2023\24 amekuwa kinara wa ufungaji bora akifunga mabao 21. Akiwa katika vita vikali na nyota wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, akishika nafasi ya pili akitikisha nyavu mara 19.