OKRA: JANGWANI PAMEKUWA PACHUNGU, HAPAKALIKI
IMEELEZWA kuwa Yanga ipo katika hatua za mwisho na kiungo wake mshambuliaji, Mghana Augustine Okrah ya kusitisha kusitisha mkataba au kumtoa kwa mkopo ndani au nje ya nchi mwishoni mwa msimu huu.
Kiungo huyo alikuwepo katika kikosi cha Simba, katika msimu uliopita kabla ya kuomba mkataba wake uvunjwe ili aende akatafute changamoto nyingine mpya nyumbani kao Ghana, kabla ya kurejea katika dirisha dogo msimu huu.
Mghana huyo alisajiliwa na Yanga, katikadirisha dogo la msimu huu akitokea Ghana kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambacho kilitwaa ubingwa wa ligi.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa sababu ya kocha huyo kupendekezwa kuachwa, ni kushindwa kuonyesha kiwango kizuri cha kumvutia, iliaendelee kubakia hapo msimu ujao.
Aliongeza kuwa kiungo huyo anaondolewa ili wapate nafasi ya mchezaji mwingine kigeni, mwenye kiwango kikubwa zaidi ya Okrah ambaye atakuja kuongeza ushindani katika kikosi cha Gamondi.
“Okrah ameshindwa kumshawishi kocha Gamondi ili abakie kuichezea Yanga, katika msimu ujao ni baada ya kushindwa kuingia katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, msimu huu.
“Kocha amekuwa akimpa nafasi ya kucheza mara kadhaa, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango bora katika michezo ya ligi na kimataifa, hivyo uwezekano wa kubakia mdogo Yanga.
“Okrah ni mchezaji mzuri katika timu, lakini ameshundwa kuingia katika mfumo wa kocha, hivyo atampisha mchezaji mwingine wa kigeni mwenye kiwango bora zaidi yake, atakayekuja kuongeza kitu katika timu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said alizungumzia usajili wa msimu ujao alisema kuwa “Kitu kitu kuhusu wachezaji wa kuachwa na kubakia lipo kwa kocha wetu Gamondi, hivyo mashabiki wasubirie muda ukifika kocha ataweka wazi wachezaji wa kuachwa.