FT: LIGI Kuu Bara
Uwanja wa Azam Complex
Simba 2-0 Mtibwa Sugar
Goal Michael Fred dakika ya 35.
Saleh Karabaka dk 64.
Mchezo wa mzunguko wa pili ni Simba v Mtibwa Sugar kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.
Ikumbukwe kwamba Simba mchezo wake uliopita ilikuwa ugenini ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 2-2 Simba.
Kennedy Juma ambaye alijifunga kwa upande wa Simba mbele ya Namungo kwenye harakati za kuokoa hatari leo ameanza benchi huku Kazi akianza.
Mtibwa Sugar mchezo wao uliopita walishuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 2-1 Mtibwa Sugar.