KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Aziz KI ameweka wazi kuwa kuna ofa nyingi ambazo zipo mezaniki lakini kipaumbele chake cha kwanza ni timu anayoicheza kwa wakati huu.
Ipo wazi kwamba nyota huyo mkataba wake unagota mwisho mwishoni mwa msimu wa 2023/24 ambapo inatajwa kwamba miongoni mwa timu ambazo zinahitaji saini yake ni pamoja na Simba.
Mbali na Simba inatajwa kwamba Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini inavutiwa na uwezo wa kiungo huyo na ipo kwenye mpango wa kuinasa saini yake.
Ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya Yanga kutwaa ubingwa KI amefunga jumla ya mabao 18 na pasi 8 za mabao kwenye ligi.
Kwenye mchezo dhidi ya Tabora United ambao ulikuwa ni mzunguko wa pili nyota huyo alifunga bao moja dakika ya 90.
Nyota huyo amesema: “Kuna ofa nyingi ambazo zipo lakini kipaumbele changu cha kwanza ni kuwa ndani ya Yanga kwa kuwa tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kila mchezaji ni familia.
“Ninamshukuru Mungu kwa namna ambavyo tunafanya vizuri na kupata matokeo kikubwa ni kuendelea kuwa pamoja kwa kuwa kazi bado inaendelea.”