MATAJIRI wa Dar, Azam FC wameweka kambi mji kasoro bahari, Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.
Azam FC imetoka kupata ushindi wa mabao 4-1 Namungo kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali CRDB Federation Cup inakutana na Mtibwa Sugar iliyowafungashia virago kwenye hatua ya robo fainali.
Ikumbukwe kwamba Mtibwa Sugar chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila safari yake kwenye CRDB Federation Cup iligotea mbele ya Azam FC walipoteza kwenye hatua ya robo fainali.
Tayari Azam FC Jumamosi ya Mei 4 2024 walikuwa ndani ya Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Manungu, Mei 6 2024.
Mchezo uliopita Mtibwa Sugar kwenye ligi ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba hivyo inapamana kupata pointi tatu kujinasua kwenye hatari ya kushuka dara.
Yusuph Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wanawaheshimu wapinzani wao na kikubwa wanahitaji pointi tatu muhimu.
“Wapinzani wetu tunawaheshimu tupo tayari kwa ushindani kikubwa ni kupata pointi tatu muhimu,”.