INAELEZWA kuwa nyota wa Yanga ambaye ni chaguo la kwanza ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo ana ofa kibao mezani kwa timu mbalimbali kuwania saini yake.
Ni Clement Mzize anatajwa kuwa na ofa zaidi ya tatu mezani kwa timu kubwa barani Afrika kuhitaji saini yake kutokana na mwendelezo wake ndani ya uwanja kwenye mechi ambazo anapewa nafasi na Kocha Mkuu Miguel Gamondi.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mzize alitoa pasi mbili za mabao alimpa Joseph Guede na Aziz KI ambao walifunga kwenye mchezo huo.
Ukiweka kando mchezo huo Mzize alitoa pasi mbili kwenye Kariakoo Dabi, Novemba 5 2023 Yanga waliposhuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.
Miongoni mwa timu ambazo zimepeleka ofa inatajwa Azam FC huku Yanga nao wakiwa kwenye mazungumzo kumboreshea mkataba wake kwa kuwa kuna timu kutoka Ulaya inahitaji saini yake.