Klabu ya Simba imecheza Robo Fainali ya TANO juzi NNE za klabu Bingwa na MOJA ya Shirikisho, mara zote Simba amekufa KIUME.
Katika Safari ya ndoto ya Simba kwenda nusu fainali Afrika kweye uso wa mafanikio ya Yanga ambayo tayari imevunja mwiko wa Robo fainali Shirikisho na kuweka KIBAO cha Mafanikio JUU KABISA kwa kufika Fainali.
Katika Robo fainali zote alizocheza Simba kwa Mjumuisho wake alitolewa na TP MAZEMBE, AL AHYL, WYDAD, KAIZER CHIEFS, ORLANDO PIRATES, hizi ni miongoni mwa vilabu vyenye uwezo kiuchumi na kila wakati vinapigana kutafuta Ubora zaidi na zaidi, ajabu na kweli Simba ipo katika Muundo ule ule na haijashuka wala KUPANDA.
Kinachowaumiza mashabiki wa Simba wala sio Timu yao kushuka bali Ubora alionao YANGA kwa Zama hizi. Ukitazama alama zilizokua zinampa Simba Ubingwa na Kumvusha Makundi mashindanonya Afrika ni zile zile walau tofauti alama Moja au MBILI hazizidi alama TANO. Lakini Yanga amevuka ubora wa Simba kwa kuvuka zile Alama ambazo simba alikua anachuku UBINGWA.
Kinachotakiwa ni kwamba Simba WAKOMAE kuvuka Ubora wao wenyewe na kuvuka KIPIMO cha Mpinzani ambaye kwa sasa ana nguvu na Ubora zaidi yake. Matajiri wa Simba na Uongozi kuna haja ya kupigania UBORA na kwa sasa wamepata Kipimo sahihi ambacho ni Yanga, wawekeze kwenye kila NYANJA, Scouting na mambo yote muhimu ya kiutendaji na KIUFUNDI.