KIMATAIFA

NABI ANAVYOKIMBIZA KWA REKODI MPYA

Kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi anaendelea kuandika historia katika vitabu vya FAR Rabat kutokana na kukimbiza rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kukusanya pointi nyingi kwenye Ligi Kuu Morocco ndani ya misimu mitano.

FAR Rabat ni bingwa mtetezi msimu uliopita alitwaa taji hilo baada ya kukusanya pointi 67 hivyo Nabi amebakiza ponti tisa ambazo ni sawa na mechi tatu kufikia rekodi hiyo akiwa na michezo sita mkononi.

Wakati msimu wa 2021/22 Wydad ndio alitwaa taji akifanikiwa kukusanya pointi 63, mshindi wa pili ilikuwa Raja Casablanca ambayo ilikusanya pointi 59 huku FAR Rabat akimaliza nafasi ya tatu na pointi zake 45, msimu wa 2020/21 Wydad alitwaa ubingwa akikisunya pointi 67, 2019/2020 Raja Casablanca alitwaa taji kwa pointi 60. Hivyo ni wazi endapo atashinda mechi zote sita atafikisha pointi 76 na kuandika rekodi yake na kati ya hizi sita akishinda hata nne atakuwa ameandika rekodi pia kwani atavuka pointi za msimu uliopita.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button