Shirikisho la Soka la Saudi Arabia litakagua upya kanuni za maadili ya mashabiki baada ya shabiki mmoja kuonekana akimchapa viboko mchezaji wa Al-Ittihad.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mechi baada ya Al-Ittihad kufungwa na Al-Hilal katika michuano ya Saudi Super Cup mjini Abu Dhabi, ambapo Al-Ittihad ilipoteza kwa mabao 4-1.
Picha zinaonyesha mshambuliaji wa Al-Ittihad, Abderrazak Hamdallah akimrushia maji shabiki, ambaye alikuwa amempiga mchezaji huyo mara mbili kwa kile kinachoonekana kama mjeledi.
Huku shirikisho la soka Saudia ‘SAFF’ limesema “limeshtushwa na matukio hayo ya aibu”.
“Kandanda nchini Saudi Arabia ni mchezo wa familia na, tunashukuru, machafuko ya mashabiki ni nadra sana,” SAFF ilisema.
“Ndio maana vitendo vya shabiki ”huyu” vinaenda kinyume na yote ambayo soka la Saudia linawakilisha na tunalaani vikali tukio hilo.”Kutakuwa na ukaguzi wa kina wa maadili ya mashabiki. Ukaguzi huo utahakikisha sheria na kanuni zilizoboreshwa zinawekwa ili kutoa adhabu kwa haraka ili kuzuia kurudiwa kwa matukio kama haya.”