LIGI KUU BARA KIVUMBI KINGINE LEO
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni mzunguko wa pili kwa msimu wa 2023/24.
Aprili 26 ikiwa ni kumbukizi ya miaka 60 ya Muungano mchezo mmoja unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Dodoma Jiji ambao ni wenyeji watawakaribisha KMC kwenye mchezo huo wa mzunguko wa pili kusaka pointi tatu muhimu.
Dodoma Jiji kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 10 na pointi 25 kibindoni inakutana na KMC iliyo nafasi 5 ikiwa na point 32 kibindoni.
Wazir Junior, mshambuliaji wa KMC kuelekea kwenye mchezo huo amebainisha kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuona wanapata matokeo mazuri mbele ya wapinzani wao.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunaamini wapinzani wetu ni timu imara lakini tutapambana kufanya vizuri na kupata matokeo,”.