KOCHA wa Azam FC, Youssouph Dabo ametaja wachezaji watano kutoka Yanga na Simba ambao amewapendekeza kwa uongozi wa timu hiyo kuhitaji huduma zao kwa ajili ya msimu ujao wa Mashindano.
Amewataja wachezaji hao kutoka Yanga ni kipa Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki ambaye mkataba wake unatamatika mwishoni na msimu huu na Clement Mzize ambaye majuma yaliyopita aliongeza mkataba wa miaka miwili ambapo kila mwezi kupokea mshahara wa laki saba.
Kwa upande wa Simba alimtaja Clatous Chama ambaye naye mkataba wake upo ukingoni na Kibu Denis kwa ajili ya kutaka kuimarisha kikosi chake kwa msimu wa 2024/25.
Kocha Dabo amesema amewafatilia wachexaji hao wako vizuri na tayari majina amependekeza kwa uongozi wapo kwenye mipango yao ya usajili kwa ajili ya kuboresha timu yao msimu ujao wa Mashindano.
Amesema majina hayo amewapendekeza kwa uongozi wa timu hiyo kuhakikisha wanaganikiwa kupata saini ya wachezaji ambao anawahitaji kwa msimu ujao.
“Sio Mzize pekee ndio tunataka bali kuna Diana na Aziz Ki pale Yanga, Simba tunahitaji wachezaji wawili Chama na Kibu. Wachezaji wazuri mambo yakienda vizuri ninaimani tutapata huduma za nyota hao,” amesema Dabo.
Kuhusu suala la ubingwa msimu huu, amesema kulingana na muelekeo wa timu yake wako katika reli ya kuwania taji hilo kutokana na tofauti ya pointi 4 kati ya aliyekuwa juu yao ambao ni Yanga.
Katika msimamo Azam FC wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 54 wamecheza michezo 24 na Yanga wakiongoz ligi kwa pointi 58, kwa michezo 22 huku Simba nafasi ya tatu kwa alama 46 amecheza michezo