LICHA ya mazingira ya Uwanja wa Meja Isamuhyo kutokuwa rafiki kwa timu zote mbili ngoma imekuwa ngumu kwa wote wawili kugawana pointi mojamoja.
Ubao umesoma JKT Tanzania 0-0 Yanga baada ya filimbi ya mwisho kwa mwamuzi kupigwa katika mchezo wa mzunguko wa pili.
Ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza JKT Tanzania walishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Yanga 5-0 JKT Tanzania leo wamefanikiwa kutoruhusu bao na kupata pointi.
Ni pointi 59 wanafikisha baada ya kucheza mechi 23 Yanga huku JKT Tanzania ikifikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi 23 ikiwa na wastani wa kuvuna pointi moja kila mchezo.