WAJEDA JKT Tanzania wanatarajiwa kuwa na kazi nyingine kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.
JKT Tanzania mchezo wake wa mzunguko wa pili uliopita ilikuwa dhidi ya Yanga na ilishuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 0-0 Yanga.
Katika mchezo huo waligawana pointi mojamoja baada ya dakika 90 kukamilika kwa kuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-0 JKT Tanzania.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ikiwa ni msako wa pointi tatu muhimu kwa kila mmoja kuwa kwenye kazi ya kusaka pointi tatu.
JKT Tanzania kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 23 inakutana na Mtibwa Sugar yeye pointi 17 baada ya kucheza mechi 22.