UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa suala la usajili ni sanaa hivyo ni lazima anayefanya jambo hilo kujua ni kitu gani anakifanya kwa wakati huo.
Ni Rais wa Yanga, Injnia Hersi Said amebainisha kuwa ni lazima kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kukamilisha usajili jambo ambalo ni muhimu kuzingatia katika kutimiza majukumu hayo.
“Usajili ni sanaa, ni lazima ujue kwanini unafanya huo usajili. Kwa kifupi huwezi kubaki na wachezaji wako wazuri kwa muda wote, hivyo inabidi utengeneze mazingira mazuri ya kuvutia Wachezaji wengine wazuri. Hivyo nilichukua maamuzi ya kusimamia mchakato wa usajili.
“Unapokuwa kiongozi lazima uwe na maono makubwa sana na uelewa mkubwa wa mpira.
Unapaswa kujua mchezaji yupo kwenye kilele cha ubora wake, anapata wakati mgumu kuzuoea mazingira, amechoka nk. Usipokuwa na uelewa wa mpira basi utajikuta unasajili hovyo au unatimua wachezaji kwa hisia,”.
Miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Yanga na kuleta matokeo mazuri hivi karibuni ni pamoja Aziz KI ambaye ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao 15 ndani ya ligi.
Nyota huyo anafanya kazi kubwa kwa ushirikiano na Yao, Kibwana Shomari na Dickson Job pamoja na wachezaji wengine ndani ya kikosi cha Yanga.