Mchambuzi mkongwe wa soka nchini, Shaffih Dauda amesema kuwa YANGA wananafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo dhidi ya Mamelod ya Afrika kusini kuliko watani zao Simba watakaocheza na Al Ahly ya Misri.
Leo Simba na Yanga zitakuwa kwenye kibarua kingine kigumu cha kujaribu kuweka historia mpya kwenye soka la Tanzania kwa kufuzu kwa mara ya kwanza kwenda hatua ya Nusu Fainal.
“Mimi nitakuwa tofauti kidogo, sioni Simba wakisonga mbele dhidi ya Al-Ahy Mchezo walipaswa kuumaliza kwa Mkapa. Al-Ahly waliwasoma Simba kuwa huwa wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani wakaimaliza mechi.. Simba ni Watanzania wenzetu lakini ukweli mchingu ni huo”
“Wote tulikuwa Loftus Versveld, nimemuona Aucho na Pacome wana train na wana ari ya kupambana japo Pacome alikuwa ana train peke yake. Kwangu mimi naishauri Yanga isicheze kama walivyocheza Dar.. Approach ya Mchezo wa kwanza ilikuwa nzuri sana lakini hapa nyumbani kwao Mamelodi Sundowns hushambulia sana”
“Yanga wanaweza kupishana, ningemshauri kocha, Gamondi awashambulie Mamelodi, asikae nyuma kuwasubiri kwani wataleta mafuriko ya mashambulizi. Sidhani kama Mamelodi watashindwa kufunga goli, Yanga akishambulia pia anweza kupata goli.. Sare yoyote ya magoli Yanga anapita.”
“Mechi ni ngumu lakini Mamelodi wananafasi kubwa ya kushinda. Kama nilivyosema awali Yanga hatuwadai, lengo lilikuwa makundi lakini wako robo fainali hawapaswi kuwaogopa Mamelodi, wawashambulie kwani hiyo quality wanayi, hawana cha kupoteza lolote laweza kutokea.”