MWAMBA Aziz KI kafanya kazi kubwa ndani ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns dakika zote 180 wakitoshana nguvu uwanjani na kuondolewa kwa changamoto za penalti.
Yanga imeonyesha ukomavu mkubwa katika mechi zote mbili hakika wanastahili pongezi kwa kazi kubwa mbele ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Kwenye changamoto za penalti ilikuwa Mamelod 3-2 Yanga jambo lililofanya wakagotea kwenye hatua hiyo. Leo kikosi kinatarajiwa kurejea Dar kwa maandalizi ya mechi zinazofuata katika Ligi Kuu Bara na CRDB Federation.
Mwamba Aziz Ki bao lake dhidi ya Mamelodi Sundowns lilikataliwa kutokana na VAR katika mchezo ambao walikuwa katika ubora. Mwamba Aziz KI anatajwa kuwa katika rada ya vigogo mbalimbali Afrika wakihitaji saini yake.
Yanga wameonyesha wanakitu kuanzia hatua ya makundi mpaka robo fainali bado wachezaji wanajituma na kushirikiana kufanikisha malengo jambo ambalo limewafanya wawe hapo.
Nidhamu kwa benchi la ufundi pamoja na uwepo wa mashabiki ni miongoni mwa nguzo ambazo zinawapa nguvu kuwa hapo walipo hivyo wana muda wakujipanga kurejea kwenye ubora wakati ujao.