Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuacha makasiriko na badala yake waungane Pamoja kuisaidie timu yao ifanye vizuri katika mechi zilizosalia ikianzia mechi ya tarehe 20 dhidi ya watani zao Yanga SC.
“Tuna timu bora sana lakini tumekuwa tukiadhibiwa kwa makosa ya kujirudia, kuruhusu goli kila mechi, sina uhakika tuna clean sheets ngapi msimu huu. Makosa ya kutotumia nafasi ipasavyo yamekuwa yakitugharimu.
“Hata tukicheza na katimu kadhaifu kiasi gani, tukikafunga bao nyingi lazima katatufunga hata bao 1.
Hii ndiyo sehemu inayotugharimu. Mechi ya Ihefu tumetengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha kwanza lakini tulishindwa kuzitumia, tungeweza kutoka hat aba bao 4.
“Tukiondoa makosa hayo katika michezo 10 iliyosalia kuanza na huu wa Yanga, ninaamini Simba anakwenda kutakata Benjamin Mkapa.
“Simba haijawahi kupoteza mara mbili kwenye msimu mmoja kwa mpinzani mmoja, hivyo itakuwa ajabu kwa Simba yetu sisi kupoteza mbele ya Yanga mara mbili ndani ya msimu mmoja.
“Ukweli usemwe, mechi ya Aprili 20 ni mechi ngumu kwelikweli kutokana na form aliyonayo mpinzani wetu inampa ushindi, ana ile winning mentality, anashinda mechi zake anapata anajiamini na ana ujasiri kuelekea mchezo wetu.
“Tunatakiwa tukajipange kwelikweli kana kwamba mechi hiyo ni ya mwisho kwenye masiha yetu. Haituogopeshi lakini inatupa nafasi ya kuelekea mchezo huo,” amesema Amhed Ally.