UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa licha ya ubora ambao walikuwa nao wakipoteza mbele ya Al Ahly wana nafasi ya kufanyia kazi makosa yao kuelekea mchezo wa marudio Cairo, Misri.
Ikumbukwe kwamba ni mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya robo fainali kete ya pili inatarajiwa kuchezwa Misri Aprili 5, ambapo hatma ya nani atasonga mbele itafahamika, huku simba wakihitajika kufunga angalau Gori 2 na kutoruhusu nyavu zao kutikiswa ili waifikie historia wanayoiota ya kuingia nusu fainali.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema: “Tumepoteza mchezo katika siku tuliyokua bora sana kiwanjani. Nafasi nyingi tumetengeneza nafasi nyingi tumepoteza, Huo ndio mpira.
“Bado tunayo nafasi ya kuipambania timu yetu katika mechi ya marudiano. Malengo yetu ni yale yale Nusu Fainali. Hakuna kukata tamaa mechi ya marudiano itaamua sisi au wao. Poleni wana Simba vita bado inaendelea,”.