MWAMBA Pacome Zouzoa kiungo wa Yanga aliwavuruga Waarabu wa Algeria CR Belouizdad kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa kutokana na kasi yake na pasi za uhakika akitumia zaidi mguu wake wa kulia.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 4-0 CR Belouizdad katika mchezo wa hatua ya makundi ikitinga hatua ya robo fainali na mchezo wake wa kufungia kazi kwenye makundi ilipoteza dhidi ya Al Ahly 1-0 Yanga.
Mabao kwenye mchezo dhidi ya Waarabu wa Algeria yalifungwa na Mudathir Yahya, Kennedy Musonda, Aziz KI na Joseph Guede ambaye bao lake la dakika ya 84 liliwapa uhakika Yanga kutinga hatua ya robo fainali.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Februari 24 Pacome kwa kususika kwenye miguso zaidi ya 60 ambapo alitumia mguu wa kulia kutoa jumla ya pasi 37, pasi tatu kwa mguu wa kushoto, alikokota mpira mara 15 na alipiga mashuti yaliyolenga lango mawili miguso kwa kichwa ilikuwa mara mbili alitoa pasi moja ya bao kwenye mchezo huo.
Katika pasi alizotoa kwa mguu wa kulia ni nne pekee hazikuwafikia walengwa aliokuwa akiwapa ndani ya uwanja alipokomba jumla ya dakika 90 kwenye mchezo huo.
Ukiweka kando Pacome mwenye mabao matatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, kipa Djigui Diarra langoni aliokoa hatari saba ilikuwa dakika ya 4, 16, 45, 60,66, 85 na 88.
Pacome amesema kuwa ni furaha kwa timu kiujumla kwa malengo yao kupata ushindi pamoja na mashabiki kupata furaha waliyokuwa wakiifikiria kwa muda mrefu.
“Tulikuwa tunahitaji ushindi na tumepata kwa kilichotokea kwetu ni furaha, tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu ambao ulikuwa ni muhimu kupata ushindi,”.