NAHODHA Msaidizi wa Simba SC, Shomari Kapombe amesema wachezaji wa Simba wamejiandaa vizuri kuelekea kuwakabili Al Ahly SC na wana imani wataenda kupata matokeo chanya kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema wamekuwa na wakati mzuri wa maandalizi tangu walipokuwa Zanzibar, hivyo kikosi hicho kipo kamili kupambana katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu ninaawaambia mashabiki wa Simba kuwa waje, tumejiandaa kuonesha mchezo mzuri na kushinda mechi,” amesema Kapombe.