Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said amemvaa Haji Manara baada ya kumsifia mtangazaji wa soka wa Azam TV, Gharib Mzinga.
Jemedari amesema kuwa alichokifanya Manara ni jitihada zake za kutaka kumshusha mtangazaji Baraka Mpenja huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugomvi kati ya Manara na Mpenja.
“Huyo Pablo aliyehama kutoka Manara Tv kwenda kwa Mpenja TV ndio chanzo kikuu cha ugomvi na sio kwamba ni suala la yeye akitangaza mechi za Yanga Yanga inafungwa..
“KALIKONJI alianza kumtumia sana meseji Mpenja na Mpenja akawa hazijibu ikabidi ampigie kabisa, katika maongezi kama kawaida akampa vitisho mpaka vya kumharibia kazini kwake na kujitapa kuwa ana hela ya kumlipa yeye na kununua hiyo Tv yake.
“Baada ya hapo akahamia Instagram kumpamba MZINGA na kumchafua Baraka Mpenja ili aonekane hafai mbele ya Wanayanga. Uzuri uongozi wa Yanga umemkana KALIKONJI kupitia msemaji wao Ally Kamwe ambaye ametoa maneno ya kuwataka Wanayanga kumuunga mkono Baraka Mpenja
“Mzinga anapaswa kuwa makini na KALIKONJI, atakujaza maneno laghai yule lakini baadae akishindwa kukutumia atakugeuza adui na kusema yeye ndiye kakufikisha hapo na maneno ya kijinga mengi, take care bro.
“Mpenja na Mzinga fanyeni kazi zenu huu ni wakati wenu kila mmoja ana mashabiki wake wanaompenda na kumsapoti sana hakikisheni hakuna mtu anayewagomanisha.”