KITAIFA

GAMONDI BABA LAO LIGI KUU KWA SASA

Unaambiwa Kocha mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa mwezi Februari Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha Gamondi amekiongoza kikosi cha Young Africans katika michezo mitano mwezi na kufanikiwa kushinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja sambamba na kuiwezesha klabu hiyo kutoka nafasi ya pili hadi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi.

Young Africans ilitoka 0-0 na Kagera Sugar, ikazifunga Dodoma Jiji bao 1-0, Mashujaa 2-1, Prisons 1-2 na KMC 0-3.

Gamondi amewashinda Abdelhak Benchikha wa klabu ya Simba na Ahmad Ally wa Tanzania Prisons alioingia nao katika kinyang’anyiro hicho.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Azam Complex, Amir Juma kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Februari.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button