KITAIFA

AZAM FC YAKOMBA POINTI TATU ZA YANGA

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamekomba pointi tatu mazima kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Azam FC 2 -1 Yanga.

Mabao ya yamefungwa na Feisal Salum dakika ya 51 na Gibril Sillah dakika ya 19 kwa Azam ni Clement Mzize kwa Yanga dakika ya 10.

Mzunguko wa pili ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo ule wa kwanza ni Yanga walikomba pointi tatu.

Kwenye mchezo wa Machi 17 2024 kadi 7 za njano zimetolewa huku Azam FC wachezaji wanne na Yanga wachezaji watatu walionyeshwa Kadi za njano na mwamuzi wa kati.

Pacome Zouzoua alipata maumivu na kutolewa kwa mabadiliko ya lazima nafasi yake ilichukuliwa na Guede.

Kwa pointi hizo tatu, Azam FC inafikisha pointi 47 kwenye msimamo ikiwa nafasi ya pili na Yanga wanabaki nafasi ya kwanza na pointi 52.

Azam FC ni mechi 21 wamecheza kwenye ligi na Yanga mechi 20.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button