UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unatambua mchezo wao ujao dhidi ya ASEC Mimosas utakuwa na ushindani mkubwa lakini wapo tayari kupata ushindi.
Alfajiri ya Jumanne kikosi cha Simba kilianza safari kutoka Tanzania kuelekea Ivory Coast kikiwa na jumla ya wachezaji 22 pamoja na benchi la ufundi.
Ni Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha yupo na kikosi hicho akishirikiana na makocha wengine kwa ajili ya kuwapa mbinu wachezaji waliopo kwenye timu hiyo ikiwa ni pamoja na Aishi Manula, Ally Salim, Hussen Abel kwenye upande wa makipa, Mohamed Hussen, Che Malone kwa upande wa ulinzi.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally ameweka wazi kuwa wataanza mazoezi jioni ya leo Februari 21 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.
“Wachezaji na benchi la ufundi wamefika salama hilo tunamshukuru Mungu ambacho kipo kwa sasa ni maandalizi kwa mchezo wetu dhidi ya ASEC Mimosas na tutaanza maandalizi mapema kwa kufanya mazoezi tukiwa hapa,”.
Mchezo huo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Februari 23.